Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete, anatarajiwa kukabidhi nyumba 36 kwa waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki,amesema kuwa Rais Kikwete atakabidhi nyumba hizo zilizojengwa na Serikali ya Tanzania kwa ajilia ya waathirika wa mabomu ya gongo la mboto, nyumba hizo zimejengwa katika maeneo ya Msongola Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
Aidha Sadiki alisema kuwa shughuli ya makabiziano ya nyumba hizo kwa raia walioathirika na uripukaji wa mabomu katika kambi ya kijeshi iliopo mbagala yatafanyika katika maeneo yaliojengwa nyumba hizo huko msongola katika halmashauri ya manispaa ya ilala
Kwa upande wa Serikali ya tanzania imeona ni bora kuchukua hatuwa ya ujenzi wa nyumba mpya kwa watu hao kutokana na kile kitendo kilichotokea mwezi februari 18, mwaka jana cha milipuko ya mabomu katika kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) iliyoko Gongo la Mboto na kusababisha vifo vya watu takribani 30 na wengine 600 kujeruhiwa.
kutokana na hali hio watu kadhaa walikosa makaz yao ya kudumu hatuwa hii ya kukosa makaazi ilikuja baada ya watu hao kuharibiwa vibaya nyumba zao walizokuwa wanaishi na miripuko hio,kutokana na taarifa ya tathmini zilizofanywa zinaeleza kwamba nyumba 77 ndio zilizoharibika na 1,748 ziliathirika kwa uchache mdogo sana.
Tuesday, December 11, 2012
Rais kikwete kukabidhi nyumba kwa waathirika wa mabomu ya gongo la mboto.
2:15 PM
Hamed Mazrui
No comments
0 comments:
Post a Comment