Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam imeambiwa na shahidi wa pili, Ismail Juma (49), kwamba Baraza la Maulamaa lilibariki Kampuni ya Agritanza kumiliki eneo la Waislamu lililopo Chang’ombe Markas, wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam.
Kadhalika Mahakama imeambiwa kwamba Kampuni ya Agritanza inamiliki eneo hilo kihalali na walilipata kupitia njia halali tofauti na madai ya katibu Mkuu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda (54), na wenzake 49 wanaodai eneo hilo limevamiwa isivyo halali.
Sheikh Ponda na wenzake wanakabili na mashtaka matano, kula njama, kuingia, kujimilikisha ardhi kwa jinai, wizi wa mali ya Sh. milioni 59.6 na Sheikh huyo kufanya uchochezi wa kuhamasisha wafuasi
wake kutenda makosa.
Sheikh Juma ambaye ni Kadhi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, alitoa madai hayo mbele ya Hakimu Mkazi, Victoria Nongwa, wakati akitoa ushahidi wa upande wa Jamhuri dhidi ya Sheikh Ponda na wenzake.
Akifafanua zaidi, shahidi huyo alidai kuwa Baraza la Maulamaa ni chombo cha Juu kinachoundwa na wajumbe kutoka mikoa yote ya Tanzania na kwamba linatoa maamuzi ya mwisho chini ya miongozo mbalimbali kwa Waislamu.
“Januari 3, mwaka 2011 tulifanya kikao cha Maulamaa na ajenda kuu ilikuwa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Kiislamu, iliamriwa chuo kijengwe Chang’ombe, lakini ikaonekana chuo hicho kinahitaji sehemu kubwa sio eneo hilo lenye heka 4…Katibu Mkuu na tume ya baraza letu walipewa jukumu la kutafuta eneo la kutosha,” alidai shahidi huyo na kuongeza:
“Baada ya siku tano kupita, tulipokea simu tukihitajika kwenye kikao cha dharula… tulikutana na Katibu Mkuu, alitoa taarifa ya kupatikana eneo na kwamba Kampuni ya Agritanza inataka kutoa eneo la heka 40 lililopo Kisarawe mkoani Pwani kwa kubadilishana na eneo la Chang’ombe Markas,” alidai Sheikh Juma.
Alidai kuwa kutokana na taarifa hiyo wajumbe wa baraza hilo waliafiki na kuona kwamba kutoa heka nne na kupokea heka 40 ni kama mbingu na ardhi walifurahia hatua hiyo.
“Tulikubaliana baraza zima la Maulamaa na mabadiliko ya kufanya makabidhiano yakafanyika kwa Wailsamu kumiliki eneo la heka 40 Kisarawe na kampuni hiyo kuwa wamiliki halali wa eneo la Chang’ombe Markas,” alidai shahidi huyo wakati akimaliza kutoa ushahidi wake.
Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Baraza la Waisamu Tanzania (Bakwata), Ustaadhi Suleiman Lilila, aambaye ni shahidi wa kwanza, aliiambia mahakama hiyo kuwa kiwanja hicho ni mali halali ya Kampuni ya Agritanza na kwamba Sheikh Ponda na wenzake hawana haki.
Mbali na Ponda, washtakiwa wengine kuwa ni Kuluthumu Mohamed, Zaldah Yusuph, Juma Mpanga, Farida Lukoko, Adamu Makilika, Athum Salim, Seleman Wajumbe, Salum Juma, Salum Mkwasu na Ramha Hamza.
Wengine ni Halima Abas, Maua Mdumila, Fatihiya Habibu, Hussein Ally, Shaban Ramadhani, Hamis Mohamed, Rashid Ramadhani, Yusuph Penza, Alawi Alawi, Ramadhani Mlali, Omary Ismaili, Salma Abduratifu, Khalidi Abdallah, Said Rashid, Feswali Bakari, Issa Wahabu, Ally Mohamed, Mohamed Ramadhani, Abdallah Senza, Juma Hassani na Mwanaomary Makuka.
Upande wa Jamhuri uliendelea kuwataja wengine kuwa, Omary Bakari, Rashid Ndimbu, Hamza Ramadhani, Ayubu Juma,Maulid Namdeka, Farahan Jamal, Smalehes Mdulidi, Jumanne Mussa, Salum Mohamed, Hamis Halidi, Dite Bilali, Amiri Said, Juma Yassin, Athuman Rashid, Rukia Yusuph, Abubakari Juma na Ally Salehe.
Upande wa huo wa mashtaka ulidai kuwa katika shtaka la kwanza, Oktoba 12, mwaka huu huko Temeke jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote 50 walikula njama ya kutenda makosa.
Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa siku ya tukio la kwanza, eneo la Chang’ombe Markas, wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote 50 kwa jinai walivamia kwa nia ya kutaka kujimilikisha kiwanja mali ya Agritanza Ltd.
Ilidaiwa katika shtaka la tatu kuwa, kati ya Oktoba 12 na 16, mwaka huu Chang’ombe Markas pasipo uhalali na hali ya uvunjifu wa amani washtakiwa wote kwa pamoja walijimilikisha ardhi ambayo ni mali ya Agritanza Ltd.
Shtaka la nne, ilidaiwa kuwa kati ya Oktoba 12 na 16, mwaka huu Chang’ombe Markas washtakiwa wote kwa pamoja waliiba vifaa mbalimbali vya ujenzi ikiwamo matofali 1,500, tani 36 za kokoto na nondo vyote vikiwa na thamani ya Sh. 59,650,000 mali ya Agritanza Ltd.
Shtaka la tano linamkabili Sheikh Ponda na Sheikh peke yake, kati ya Oktoba 12 na 16, mwaka huu Chang’ombe Markas, wilaya ya Temeke, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa Katibu wa Baraza la Waislamu Tanzania, aliwashawishi wafuasi wake kutenda makosa ya jinai.
Washtakiwa wote walikana mashtaka yao kwa nyakati tofauti.
Aidha Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), amewasilisha hati ya kiapo ya kuzuia dhamana ya mshtakiwa wa kwanza Sheikh Ponda na watano Mukadam Swalehe (45) kwa sababu ya usalama wao na maslahi ya taifa.
Hali ya ulinzi mahakamani hapo ulikuwa mkali na kwamba kila aliyeingia katika viunga alifanyiwa upekuzi na vifaa maalum na makachero.

CHANZO: NIPASHE
0 comments:
Post a Comment