Sunday, December 16, 2012

SUZA TO CELEBRATE ITS EIGHTH GRADUATION CEREMONY

 
The State University of Zanzibar (SUZA) will celebrate its eighth graduationceremony on Saturday 22 nd
December, 2012.
 
The event will take place in its newCampus premises at Tunguu, Central District, Zanzibar South around 08.30 a.m. HisExcellency, Dr. Ali Mohamed Shein, the President of Zanzibar and the Chairman of the Revolutionary Council who is also the Chancellor of the State University of Zanzibar is expected to confer and present degrees, diplomas and certificates to the2011/2012 University graduands.
 
In this year’s graduation ceremony a total 494 graduands out of which 262(53.03%) being females and 232 (46.96%) male graduands will graduate in nine (9)different academic disciplines of Certificate in Computer Science, Certificate of Information Technology, Certificate in Librarianship and Information Technology,
Graduation     Diploma in Computer Science and Diploma in Languages with Education.
 
 
 Others areDiploma in Science with Education, Bachelor of Arts with Education, Bachelor of Science with Education and Bachelor of Science in Computer Science. SUZA iscurrently running thirteen (13) academic programmes in addition to PhD in Kiswahili,Diploma in Educational Leadership and Management, Diploma in Social Work andUniversity Qualifications Framework (Level 6) Certificate from the above mentionedprogrammes.The State University of Zanzibar has this academic year increased its numberof students who have finalized their studies compared to the last academic year asduring the previous graduation ceremony a total of 320 (155 – 48.43% females and165 – 51.56% males) graduated in six (6) different academic disciplines
 
BACKGROUND INFORMATION
 
The State University of Zanzibar (SUZA) was established by Act No. 8 of 1999 of theHouse of Representatives of Zanzibar and became operational on 26
th
September,2001.
 
The University has recently undergone a massive restructuring process movingfrom having the School of Education, Arts and Sciences (SEAS) and two (2) Institutesof Kiswahili and Foreign Languages (IKFL) along with the Institute of Continuing Education (ICE) which existed for a decade to four (4) recently introduced Schools of Kiswahili and Foreign Languages, Natural and Social Sciences, Education and that of    Continuing and Professional Education.
 
Apart from these Schools, there is oneDirectorate of Library Services and several academic departments and centres Somany other envisaged programmes are to be introduced in the near future.

MATOKEO YA MAONI JUU YA KATIBA MpYA SHEIA YA MIKUNGUNI

Mwendelezo huo wa maoni juu ya katiba mpya uliendelea tena jioni ya leo huko katiaka shehia ya mikunguni na wananchi kupata fursa yao ya kutoa maoni juu ya katiba hio mpya, waliotaka Muungano huu uliopo kati ya Zanzibat na Tanganyika uendelee kama ulivo ni 41.

Na kwa upande wawananchi waliotaka Zanzibar huru kitaifa na kimataifa ikifuatiwa na Muungano wa mkataba kati yake na Tanganyika ni 91

MATOKEA YA MAONI JUU YA KATIBA MPYA KATIKA SHEHIA YA KILIMA HEWA ASUBUHI YA LEO.

kufuatia mwendelezo wa maoni juu ya katiba mpya ulioendelea tena asubuhi ya leo katika shehia ya kilima hewa wananchi waliopata  fursa ya  kutoa maoni yao ni kama hivi ifuatavo.

Waliotaka mfumo huu uliopo wa muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika uendelee kama ulivo ni 53
Na  kwa upande wawananchi waliotoa maoni yao na kutaka Zanzibar huru na yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa ikifuatiwa na muungano wa mkataba ni 71.

Saturday, December 15, 2012

Mnara wa kuongezea meli wa Ras Kigomasha wakaguliwa



AFISA Mdhamini Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Pemba Al-hajjat Jokha Khamis Makame akipanda mnara wa kuongozea meli uliopo Kigomasha Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, anaeshuka ni Mkurugenzi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Zanzibar, Naimu Ramadhan Pandu wakati ujumbe huo ulipofika huko kwa ajili ya kuangalia utendaji wa kazi wa mnara huo (picha na Haji Nassor, Pemba
picha na Haji Nassor, Pemba

LA UAMSHO NA UKIMYA WETU MSIDHSANI NDIO MMETUN YAMAZISHAZISHA


DSCF1963
Hadi sasa jeshi la polisi na serikali za Zanzibar na Tanzania zinataka iaminike kwamba viongozi wa Jumuiya ya Uamsho wanaowashikilia kwa zaidi ya mwezi sasa, ni washukiwa wa uhalifu. Uhalifu upi? Fujo, vurugu, kuharibu mali na matusi, angalau kwa kutaja machache. Wanataka sana hilo ndilo limezeshwe kwenye akili zetu. Kila mtu aimbe wimbo huo na mwisho wa siku, sote tuingie kwenye kapu moja la uzembe na uvivu wa kufikiri.

Lakini shukurani kwa mifumo ya sasa ya kimawasiliano, serikali na vyombo vyake wametukuta wengi wetu tukiwa hatudanganyiki tena na ulaghai wake. Hata kama tunaweza tusiwe na nguvu za kimabavu ilizonazo serikali, maana sisi hatuna polisi, jela wala mahakama, lakini tuna nguvu ya dhamira zetu. Nayo ni nguvu kubwa, kwa hakika.

Kwa nguvu hiyo, ya kuwa na akili huru, ndipo tunakataa kuumeza uongo wa serikali wa “kuwahalifisha” viongozi wa Uamsho na wafuasi wao. Tunajua – kama inavyojua hiyo serikali na vyombo vyake – kwamba viongozi wa Uamsho wanaadhibiwa kwa sababu ya msimamo wao wa kisiasa. Msimamo wa kuitaka Zanzibar yenye mamlaka kamili, nje ya Muungano.

Ikiwa kuna kosa lolote ambalo leo hii limemfanya Sheikh Msellem Ally ajikute akishindwa kumuuguza na hatimaye kumzika mwanawe mzazi, ni hilo la kwamba ni kiongozi aliyewaongoza Wazanzibari kuidai haki yao ya kuwa huru, heshima yao ya kujiamulia na dhamira yao ya kusonga mbele kama taifa.
Kwa kufanyiwa wanayofanyiwa viongozi wa Uamsho, serikali na vyombo vyake wanajidanganya kwamba wanalizima vuguvugu lililokwishapamba moto la Wazanzibari kudai mamlaka kamili ya nchi yao.

Na hili la upande wa serikali na mawakala wake linaweza kuelezeka ingawa halikubaliki. Lakini ambalo haliwezi kuelezeka, kukubalika, wala kuvumilika ni hili la kimya chetu sisi wengine, ambao tunaguswa na dhamira wanayoisimamia akina Sheikh Msellem.
Kwa sababu ya kutotaka kuitwa Uamsho, mimi na wenzangu wengi, tumeshindwa hata kuandika mistari miwili mitatu ya kusimama na viongozi hawa. Tunawaachia waadhibiwe, wateswe, wadhalilishwe kimwili na kisaikolojia. Kama nilivyosema hapo kabla, inawezkena hatuna nguvu za kuwanusuru na mkono dhalimu wenye nguvu wa dola, lakini tunao uwezo wa kuwahuisha mbele ya makini za watu: kuwasafishia majina na kuzitukuza thamani zao, kwa kutokubali “kuununua” uzushi dhidi yao.

Hawa si magaidi, si mahaini, si majambazi, na kwa hakika hata si wahalifu. Hawapo walipo sasa kwa sababu wameiba, wameua au wamemdhulumu mtu. Wapo walipo kwa kuwa wanapigania nchi yao – heshima ya taifa lao. Hawa ni wa kutukuzwa si wa kupewa mgongo! Si wa kupigwa pande!

Na Mohammed Khelef Ghassany

UKOSEFU wa uwelewa wa sheria ya matumizi bora ya Ardhi kumechangia ni miongoni mwa sababu za uharibifu wa mazingira.

UKOSEFU wa uwelewa wa sheria ya matumizi bora ya Ardhi kumechangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira katika maeneo ya miji na vijiji hapa Zanzibar.
 
Akiwasilisha mada kwa wanajumuiya mbalimbali, NGO’S, na Sibios huko katika ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Chakechake  Mtaalamu kutoka Idara ya Ardhi Mipango Miji na Vijiji Zanzibar nd.Muhammed Habib amesema sehemu muhimu za miji na vijiji zilizotengwa kwa ajili ya shughuli za rasilimali mbalimbali zimevamiwa kwa kujengwa hali ambayo imepoteza ramani ya miji.
 
Alisema kutokana na hali hiyo Serikali kupitia idara ya Ardhi na mipango miji inakusudia kuandaa mpango miji kwa Unguja na Pemba ili kuirejesha miji katika hali inayokubalika .
 
Aidha muhammed alisisitiza haja ya kulinda maumbile asili , rasilimalimali zisizorejesheka , maeneo muhimu ya kilimo pamoja na maeneo mengine ambayo ni muhimu kwa shughuli za uwekezaji.
 
“Nchi yetu inaigiza kipato kupitia sekta hii ya utalii sasa endapo tutaiharibu sehemu za vivutio vya watalii itafika pahala tutakuwa na uhaba wa wageni na kupelekea kudorora kwa sekta hii ambayo inaingiza kwa kiasi kikubwa hapa nchini kwetu ”Alisema mtaalamu huyo
 
Hata hivyo alisema si jambo zuri kufanya mabadiliko ya matumizi ya Ardhi na uvunaji wa rasilimali katika maeneo ya misitu hifadhi kwani kunaweza kupoteza haiba ya misitu hiyo.
 
“Maeneo ya kilimo yanahitaji kulindwa hasa tukijuwa kuwa eneo kubwa katika kisiwa cha Pemba ni kilimo na ndimo kwenye vianzio vingi vha maji sasa kabla ya kuyatumia maeneo haya kuweko na mpango maalum utakaotufanya tusiharibu maeneo hayo”alisistiza muhammed
 
Akitoa mchango mshiriki katika warsha hiyo Nd. Ali Hammad kutoka Jumuiya ya Uzalishaji wa karafuu Zanzibar amesema lazima iandaliwe mikakati madhubuti ya sera ya matumizi ya Ardhi ili kuweza kuondoa migogoro kati ya taasisi moja na nyengine .
 
Nae abdallah Khamis kutoka Jumuiya ya ufugaji Wilaya ya Wete alisema sehemu ambazo hazijafikiwa na miradi zinatumiwa vibaya hasa zile ambazo zipo zipo karibu na mito ambapo ndimo sehemu muhimu kwa vianzio vya maji
 
Warsha hiyo ya siku moja imeandaliwa na Idara ya Ardhi na Mipango miji Zanzibar imejadili mada kadhaa ikiwemo Mpango wa matumizi ya Ardhi Kitaifa na Malengo ya Matumizi ya Ardhi Zanzibar 
 
NA HAJI NASSSOR PEMBA.                                           

Mwalimu akutwa mtupu Shuleni Lindi

 
Mwalimu  Mkuu wa Shule ya Msingi Rutamba, Wilaya ya Lindi amekutwa akiwa na nguo za ndani pekee katika usingizi mzito kwenye kibao cha shule hiyo huku akiwa hajitambui kwa madai ya kilichomkutana kinahusishwa na imani za kishirikina.
Tukio hilo limetokea juzi usiku baada ya mkazi mmoja wa kijiji hicho, Juma Mbilemoto kumkuta mwalimu huyo akiwa kwenye kibao hicho wakati alipokuwa anamsindikiza nduguye,Aisha Mbilimoto aliyekuwa anasafiri kuelekea Dar es Salaam.
Akizungumzia tukio hilo, shuhuda huyo alisema alimkuta mwalimu huyo akiwa amelala chini ya kibao cha shule akiwa na nguo ya ndani tu (chupi)huku akikoroma kutokana na kuwa na usingizi mzito.Alisema awali hakumtambua mtu huyo lakini baada ya kumkaribia alimtambua kuwa alikuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo na ndipo alipochukua jukumu la kumwamsha  ili amvalishe kanga, lakini aliikataa na kuondoka kwenda nyumbani kwake akiwa kama alivyokutwa
Kwa upande wao walimu wa shule hiyo walisema kuwa, wamekosa molari wa kufanya kazi kutokana  na kitendo alichofanyiwa mwalimu mwenzao.
Akizungumza kwa niaba ya walimu wenzake mwalimu wa taaluma wa shule hiyo, Francis Milanzi alisema  walimu shuleni hapo wamekosa amani na kuwasababishia kuzihama nyumba zao  kwa muda na badala yake kwenda kukesha  kwenye ofisi za walimu tangu tukio hilo litokee.
Ofisa elimu wa Wilaya ya Lindi, Cosmas Magigi alisema amepokea taarifa za tukio hilo kwa huzuni na amewaomba walimu kuwa na subira wakati utaratibu wanalishughulikia suala hilo.
Magigi aliongeza kuwa ofisi yake itafanya utaratibu wa kumhamisha  mwalimu huyo na kumtafutia shule nyingine huku akiwataka wakazi wa eneo hilo kujenga ushirikiano na watumishi ili waweze kutekeleza majukumu yao.
Hili ni tukio la pili kutokea katika halmashauri hiyo mwaka huu ambapo la kwanza lilitokea April katika Shule ya Sekondari Ruhokwe, mwalimu wa shule hiyo alilazwa kwenye kibao cha shule  akiwa uchi wa mnyama.

MWANANCHI
 

 
Design by M.S Chopoti | Bloggerized by Ulimwengu Wa Digital