Saturday, December 15, 2012

UKOSEFU wa uwelewa wa sheria ya matumizi bora ya Ardhi kumechangia ni miongoni mwa sababu za uharibifu wa mazingira.

UKOSEFU wa uwelewa wa sheria ya matumizi bora ya Ardhi kumechangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira katika maeneo ya miji na vijiji hapa Zanzibar.
 
Akiwasilisha mada kwa wanajumuiya mbalimbali, NGO’S, na Sibios huko katika ukumbi wa Kiwanda cha Makonyo Chakechake  Mtaalamu kutoka Idara ya Ardhi Mipango Miji na Vijiji Zanzibar nd.Muhammed Habib amesema sehemu muhimu za miji na vijiji zilizotengwa kwa ajili ya shughuli za rasilimali mbalimbali zimevamiwa kwa kujengwa hali ambayo imepoteza ramani ya miji.
 
Alisema kutokana na hali hiyo Serikali kupitia idara ya Ardhi na mipango miji inakusudia kuandaa mpango miji kwa Unguja na Pemba ili kuirejesha miji katika hali inayokubalika .
 
Aidha muhammed alisisitiza haja ya kulinda maumbile asili , rasilimalimali zisizorejesheka , maeneo muhimu ya kilimo pamoja na maeneo mengine ambayo ni muhimu kwa shughuli za uwekezaji.
 
“Nchi yetu inaigiza kipato kupitia sekta hii ya utalii sasa endapo tutaiharibu sehemu za vivutio vya watalii itafika pahala tutakuwa na uhaba wa wageni na kupelekea kudorora kwa sekta hii ambayo inaingiza kwa kiasi kikubwa hapa nchini kwetu ”Alisema mtaalamu huyo
 
Hata hivyo alisema si jambo zuri kufanya mabadiliko ya matumizi ya Ardhi na uvunaji wa rasilimali katika maeneo ya misitu hifadhi kwani kunaweza kupoteza haiba ya misitu hiyo.
 
“Maeneo ya kilimo yanahitaji kulindwa hasa tukijuwa kuwa eneo kubwa katika kisiwa cha Pemba ni kilimo na ndimo kwenye vianzio vingi vha maji sasa kabla ya kuyatumia maeneo haya kuweko na mpango maalum utakaotufanya tusiharibu maeneo hayo”alisistiza muhammed
 
Akitoa mchango mshiriki katika warsha hiyo Nd. Ali Hammad kutoka Jumuiya ya Uzalishaji wa karafuu Zanzibar amesema lazima iandaliwe mikakati madhubuti ya sera ya matumizi ya Ardhi ili kuweza kuondoa migogoro kati ya taasisi moja na nyengine .
 
Nae abdallah Khamis kutoka Jumuiya ya ufugaji Wilaya ya Wete alisema sehemu ambazo hazijafikiwa na miradi zinatumiwa vibaya hasa zile ambazo zipo zipo karibu na mito ambapo ndimo sehemu muhimu kwa vianzio vya maji
 
Warsha hiyo ya siku moja imeandaliwa na Idara ya Ardhi na Mipango miji Zanzibar imejadili mada kadhaa ikiwemo Mpango wa matumizi ya Ardhi Kitaifa na Malengo ya Matumizi ya Ardhi Zanzibar 
 
NA HAJI NASSSOR PEMBA.                                           

0 comments:

Post a Comment

 
Design by M.S Chopoti | Bloggerized by Ulimwengu Wa Digital