Sunday, November 25, 2012

Al-Shabaab watolewa Beled Hawo Somalia


Wapiganaji wa al-Shabaab
Taarifa kutoka Somalia zinaeleza kuwa watu kama 12 wameuwawa katika mapigano baina ya jeshi la serikali na wapiganaji wa Al Shabaab karibu na mpaka wa Kenya.

Kamanda wa eneo hilo alisema al-Shabaab kwa muda mfupi walidhibiti mji wa Beled Hawo, ulio mpakani, kabla ya kushambuliwa na kutimuliwa.
Kila upande unadai kuwa upande wa pili umepata hasara kubwa zaidi.
Al Shabaab bado wanadhibiti maeneo mengi ya kusini na kati mwa Somalia ingawa wamekimbizwa Mogadishu awali mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by M.S Chopoti | Bloggerized by Ulimwengu Wa Digital