ASANTE MAKAMU WA KWANZA WA RAISI WA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA
Kwa kipindi cha wiki tatu mpaka nne, jukwaa la siasa za Zanzibar, zimebadilika sana
lakini kilichonivuta zaidi ni hotuba mbili za hadhara za Maalim Seif Shariff Hamad, katibu mkuu wa CUF; na VP1-SMZ/GNU.
Hotuba ya kwanza ni ile ya Kibandamaiti – ambayo hii alipasua jibu na kusema ukweli wake halisi anavyoona yeye katika mustakabali wa nchi ya Zanzibar.
Hakusita kusema ukweli hata kwa bosi wake, Rais Shein. Sitaki kusema alichokisema Maalim Seif siku hiyo, maana ukumbi huu walisoma kila kitu chake.
Hotuba ya pili, ni ile ya — mkutano wa hadhara – uwanja wa Magirisi/Mwanakwerekwe.
Hii pia ilikuwa na mantiki na maudhui yake mazito. Pia nimeona mtandao wa mzalendo, wameivisha jokho lake linalostahiki. Shukran nyote. Ah…na ile ya Amani Karume pia imenivuta sana.
Kama mtakumbuka niliwahi kusema siku moja katika mada zangu za huko nyuma kuwa kama ‘Karume + Seif ndio wangalikuwa viongozi wa GNU, basi ingalikwenda vizuri; lakini Shein bahati mbaya sana’.
Mimi nilisema haya siku hizo. Shein, amebahatika sana kuwa amepata fursa hii, na bahati hii ‘wazungu wanasema katika silver plate’ — dezo kabisa; lakini ameshindwa kuitumia fursa vizuri.
Anyway, tuache hayo. Tumuache Shein na Borafya wake na wale watukanifu wake.
Ninachotaka kusema ni kuwa sasa nimemuona Maalim Seif kuwa ni yule ninayemjua mimi – enzi zile za CUF ya kweli kweli.
Maalim Seif ‘Original au sijui nisema kuwa amekuwa ‘new born’ baada ya kupata tope tope za CCM-SMZ-GNU kwa miaka miwili iliyopita hivi.
Naam – Maalim Seif ni dhahab, hata ukiitia ndani ya tope, itangara tu.
Kwa ufupi, sasa Maalim Seif amekuwa kweli ‘Maalim Seif’ tunayemjua sisi; kwa maana kuwa anatetea haki za wazanzibari, haki za wtu wote, Uzanzibar mbele na no-nonsense. Huyu ndiye origina Maalim Seif.
Tukumbuke kuwa pia niliwahi kusema kuwa CUF inalegalega sana, lakini aliyebaki mtu pekee makini, na madhubuti ndani ya CUF ni Maalim Seif Shariff Hamad.
Yeye naona bado hajavutwa na zile stream za kisiasa za kijinga jinga ikiwemo rushwa na tamaa ya kitu; nathubutu kusema kuwa amebaki kuwa ‘clean’ guy.
Tukumbuke kuwa mkutano wa juzi Maalim Seif amegusia jambo moja kubwa sana, kuwa SMZ kupitia kwa Waziri Mwinyihaji Makame, amemwajiri ex-askari (mstaafu) kazi yake moja kubwa aliyopewa askari huyu ni ‘kupiga watu na kuadhibu watu’; na pia kumeairiwa kikundi kazi yake kama ile enzi ya mandera — mateso na kuhujumu watu in a big way!
Sasa, kweli Dr.Shein huyajui haya au ndio umeyabarik. Si kweli kama huyajui ila unayafurahia.
Muhimu ufahamu kuwa haya hayana mmoja. Wiki za nyuma tu, polisi walimkamata kijana mmoja, wakampiga na kumtesa sana.
Walidhani ni ‘UAMSHO au CUF au Mpemba’ — kumbe alikuwa ni mtoto wa Samia Suluhu Hassan (huyu waziri wa nchi Muungano).
* Kuna mwaka mmoja, askari wa JKU walimgaragiza mtu mmoja xxxx katika uchafu, wakampiga, na kumtesa vibaya sana na aina za mateso — kumbe alikuwa ndugu yake Mohammed Aboud (baba mmoja, mama mmoja). Jina .SIMJUI………..? Sasa leo Mohammed anataka kuyuambia nini? Mambo haya hayachagui mama wala baba wala mwana – ni kisago mbele kwa mbele?
Hayo yametokea na mengine, kuna wengine wale ‘virangi rangi’ zao kuu la forced marriage 1964 – wamekamatwa na kupigwa na kuteswa – kumbe wamo watoto/wajukuu wa akina Washoto, Natepe, Makungu etc.
Matokeo yake ama wameachiwa kimya kimya na lawama zimekwenda kwa Mussa Ali Mussa na timu yake; ambayo kwa sasa ajira zao ni 50-50. Wamegusa wrong line ya high tension ya umeme.
Hiyo ni mifano tu katika ufafanuzi na mifano mizuri ya hotuba ya Maalim Seif .
Mpaka kufikia kuajiriwa mtu kama huyu na kundi lake, job description yake iwe ni kupiga, kutesa na kuhujumu mali za watu – maana yake nini Dr.Shein? Kuna mipango mingi tumeisikia ya ‘maendeleo’ ikiwemo kuhuumu mali za watu (eti wapemba!) na hata kuchoma moto baadhi ya maeneno ya kibiashara – haya yoooooote tumepata tetesi na yanaingia akilini.
Dr.Shein, juzi nimekuona Dodoma ‘unatokwa na machozi’ wakati Amani Karume anazungumza. Sasa hali ya Zanzibar umeifikisha hapa: Borafya, Baraka Shamte, Vuai Ali Vuai, Seif Ali iddi, Shawana Bukheti Hassan (Mpaka mke wa VP2, mana Asha naye pia amekuwa kiongozi wa kutoa fatwa na zikatekelezwa); hebu tuambie nini role ya Second lady?
Tunajua, no doubt, role ya first lady – mama mwanawema (hii haina mjadala, she is there legally kabisa). Huyu je, wakuja mwenzangu kutoka Morogoro mji kasoro bahari?
Yeye ni nani? Hii ndio timu yako Dr.Shein, all bad boys…………! huoni aibu wala haya?
OK tuchukulie formula hii hapa: umemfukuza Mansour Yussuf Himid kazi kwa kuwa ni msemaji wa ‘anti-union’ anahoji hoji — lakini unamuacha Mwinyihaji Makame Mwadini – kufanya ujahil kama huu anaoufanya — kweli sawa hiyo.
Umemfukuza kazi Mansour kwa sababu anatetea maslahi ya Zanzibar na Wazanzibari; unamuacha Mwinyihaji just kwa sababu anawakandamiza Wazanzibari (you’re very happy on that).
Dr.Shein mimi nakushauri usikubali kupoteza fursa, na bahati uliyoipata ya kupewa GNU katika ‘silver plate’.
Kuna fununu kuwa unataka kumrejesha tena mtu kama Abdullah Rashid sijui utampa cheo gani; lakini tumepata fununu kuwa unataka kumteua Hafidh Ally Tahir (referee wa FIFA, mstaafu na kada wa CCM, na mbunge) unataka kumpa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib kuchukua nafasi ya Abdullah Mwinyi ambaye ameomba kustaafu siku nyingi tu.
Ukiwachagua hawa, na wakaungana na wenzao hao niliwataja hapo juu, kweli Zanzibar itakalika hii, si itakuwa balaa.
Kwa ihsani yake, tunakuomba uchague watu wa maana — huo utalii uliosema umeharibiwa na UAMSHO, basi ndio utakufa kabisa under Hafidh Ally, Abdullah Rashid, Shamte, Vuai, Shawana Bukheti, Mohammed Aboud (naye hajijui hajitambui, si aliambiwa kuwa yeye si Raia wa TZ kwa sababu ni Mgunya huyu n.k
HONGERA MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD “ORIGINAL’: mimi sio mwanachama wa CUF wala CCM na sitokuwa maishani kwangu kooote; lakini I rely on Maalim Seif and I trust him (only him, sio CUF wote wala CCM wote). Wengine ni ‘mushkel’ tu
MZALENDO
0 comments:
Post a Comment