Monday, November 26, 2012

BARAZA LA HABARI TANZANIA MCT LATOA MAFUNZO KWA VYOMBO VYA HABARI ZANZIBAR

Kuepo kwa misingi imara ya uongozi katika vyombo vya habari ndio jambo jambo la imara katika kufikia malengo ya sekta ya habari.

Kauli hiyo imesemwa leo katika ufunguzi wa mafunzo yalio andaliwa na baraza la habari tanziania katika ukumbi wa MCT mlendege mjin unguja.

Hayo yamekuja kufatilia kwa baadhi ya wafanya kazi katika tasisi za habari,kunyanyaswa ama kutotendewa haki na baadhi ya viongozi wao ikiwa kama kunyimwa haki ya kuzungumza wanacho kitaka pamoja na kunyimwa haki zote anazostahiki kupatiwa.

Akifungua mafunzo hayo,bw:Ali Rashid amesema kua,kuepo na viongozi imara katika idara za habari jambo pekee litakaloweza kuleta maendeleo katika idara husika na hatimae hatimae kupatikana na maendeleo kwa ujumla.

Aidha amesema kua, idara nyingi za habari zikiwemo za watu binafsi na zile za serikali,huwa hazina mjengeko wa uongozi imara na unakua na malengo tofauti na yale ya idara wenyewe,wengi wao hufanya kazi kwa maslahi yao binafsi,na hatimae kurudisha nyuma gurudumu la maendeleo hapa nchini.

Mmoja mionngoni mwa washiriki wa mafunzo hayo nd:Haji Ramadhan amesema kuwa ,ngazi nyingi za uongzi za uongozi huwa hazina sera nzuri na utekelezaji wa majukumu yao jambo ambalo linawaathiri watendaji wa ngazi za chini.

Mafunzo hayo yameshirikisha wageni tofauti wakiwemo waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali kama vile,zbc radio,zenj fm,gazeti la znibar leo pamoja na vingozi wa tasisi zisizo za kiserikali kama Mwanajamii Media Gruop.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by M.S Chopoti | Bloggerized by Ulimwengu Wa Digital