NA HAMED MAZROUY
Makamu mwenyekiti wa chama cha mapinduzi zanzibar ambae pia
ni rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi zanzibar dr ali mohd
shein amevitaka vyama vya siasa nchini kut
Oingiliana katika kutekeleza sera za vyama ili kuepusha
migogoro kwa wananchi.
Dr shein ameyasema hayo katika mkutano uliofanyika katika
uwanja wa demokrasia kibanda maiti mkutano ambao ulipata bahati ya kuhudhuriwa
na viongozi mbali mbali wa ccm kama vile balozi seif ali idi na mke wake mama
asha na miongoni mwa viongozi wengine ni bi asha rise migiro pamoja na shamsi
vua nahoza wakati alipokuwa akizungumza na wanachama na wapenzi wa ccm katika
mkutano uliofuatia sherehe za mapokezi yalionza 16-11 akitokea dodoma baada ya
kupata ushindi wa aina yake katika kuchaguliwa kuwa makamo mwenyekiti wa ccm
kwa upande wa zanzibar ambapo kabla ya hapo nafasi hiyo ilikua inashikiliwa na
rais mstaafu wa awamu ya sita ya serikali ya mapinduzi ya zanzibar dr amani
abeid karume,
Dr shein amefahamisha kuwa serikali ya umoja wa kitaifa
{suk} sio jambo geni bali ni urithi kutoka kwa marehemu abeid amani karume
ambae alikua mstari wa mbele katika kusisitiza amani, upendo, utulivu na
kuondoa ubaguzi pamoja na chuki za wenyewe kwa wenyewe hivyo chama cha ccm
kinaunga mkono suk kama ilivyowezwa kuunga mkono na dr kiketwe katika mkutano
mkuu wa nne uliofanyika dodoma..
Akizungumzia suala la uvunjifu wa amani zanzibar dr shein
amesema ikiwa yeye kama ni rais wa zanzibar anawaperemba tu wale wanaofanya
fujo, hivyo amelisifu jeshi la polisi kwa kazi kubwa walioifanya ya kurudisha
amani nchini hivyo amesema serikali itaendelea kuimarisha ulinzi amani na
utulivu na wala haitomvumilia yeyote yule atakaesababisha uvunjifu wa amani
nchini hivyo amewaomba wananchi kuacha kutumia vivuli vya dini kusababisha fujo
nchini kwani suk inatoa uhuru wa kuabudu na sio kuleta uharibifu,,
0 comments:
Post a Comment