Kwa uchache watu 10 wamepigwa risasi na kujeruhiwa mjini Garassa baada ya jeshi la Kenya (KDF) kuripotiwa kushambulia ovyo waandamanaji waliokuwa wakijaribu kuzuia magari yajeshi katika barabara ya Kisimayu yaliyokuwa yakielekea Somalia.
Wasiwasi umeendelea kuwa juu katika eneo hilo kufuatia kuuawa kwa wanajeshi wa tatu wa KDF hapo jana. Biashara kadhaa zimeendelea kufungwa na wakazi wameamua kubaki ndani ya nyumba zao wakati KDF ikifanya doria katika eneo hilo.
Jana mji huo uliwekewa amri isyo rasmi ya kutotoka nje wakati wanajeshi wakifanya ukaguzi wa nyumba hadi nyumba kuwatafua waliofanya mauaji ya askari watatu siku ya Jumatatu.
Wanajeshi hao waliouawa, walikuwa wamesimama kwa ajili ya kubadilisha tairi la gari lao kwenye karakana moja kwenye Barabara ya Kisimayu mkabala na Hoteli ya Midnimo ambapo walishambuliwa na kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana. Miili ya maofisa hao ilipelekwa kwenye Hospitali Kuu ya Garissa.
Polisi mmoja mwandamizi alithibitisha kuwa askari hao waliuweka mji wa Garissa "chini ya udhibiti". Mji huo umeshuhudia mashambulizi kadhaa ya wapiganaji wa al Shabaab tangu jeshi la Kenye lilipoingia Somalia mwezi Oktoba mwaka jana.
"Wanajeshi wako hapa kufanya ukaguzi wa nyumba kwa nyumba kutafuta silaha na rsasi. Wanashirikiana na GSU ambao wanafanya doria katika mitaa," alisema polisi huyo.
Siku ya jana, mbunge wa Dujis, Aden Duale alilalamika kuwa jeshi lilikuwa likiwasumbua raia wasiokuwa na hatia na kusema kuwa ataandaa maandamano. "Hao (al Shabaab) wameua wanajeshi watatu na sasa jeshi liko hapa kumpiga kila mtu. Lazima tupinge mwenendo wa aina hii," alisema Duale.
Biashara zilifungwa na watu wakaamuriwa kubaki ndani. Waandishi wa habari walizuiliwa kupiga picha za mitaa iliyohamwa na maduka yaliyofungwa. Hakuna magari yaliyoruhusiwa kutoka au kuingia katika mji huo.
CHANZO: THE STAR
0 comments:
Post a Comment