RAIS Jakaya Kikwete ameendelea kuteua majaji wapya licha ya madai kwamba baadhi ya majaji wanaowateua, hawana sifa.
Hivi karibuni, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, alitishia kumpeleka mahakamani Rais Kikweke, kwa madai kuwa amekuwa akiteua majaji wasiokuwa na sifa.
Jana kiongozi huyo wa nchi, aliwaapisha majaji wapya wa Mahakama ya Rufaa ambao ni Jaji Profesa Ibrahimu Juma na Jaji Bethewel Mmilla.
Kabla ya uteuzi huo Jaji Mmilla (56) alikuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, wakati Jaji Juma (54) alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria na Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, wakati Jaji Juma (54) alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
0 comments:
Post a Comment