Tuesday, November 27, 2012

Maaalim Seif ashtushwa kusitishwa huduma ya chakula Mnazimmoja


MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad ameutaka uongozi wa Wizara ya Afya kuzingatia upya uamuzi wao wa kuondosha huduma ya chakula kwa wagonjwa wanaolazwa hospitali kuu ya Mnazimmoja, kwa vile uamuzi huo unaweza kusababishia hali ngumu kwa wagonjwa wanaotoka nje ya mji wa Zanzibar ambao hawana jamaa.
Maalim Seif aliyasema hayo jana katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA), alipozungumza na wafanyakazi wa Wizara ya Afya, baada ya kumaliza ziara ya kuzitembelea taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo Unguja na Pemba.
 
Maalim Seif alihoji kwanini wagonjwa wanaolazwa katika hospitali ya Mnazimmoja wakose chakula wakati wenzao wa hospitali za Pemba wanapata milo miwili kwa siku, licha ya hali hiyo hiyo mbaya ya kibajeti iliyopo.
Nao wafanyakazi wa sekta ya afya walimueleza Makamu wa Kwanza wa Rais kuwa, miongoni mwa changamoto zinazowakabili Unguja na Pemba ni uhaba wa wataalamu na watendaji wengine katika hospitali na vituo vya Afya.
Mfanyakazi kutoka hospitali ya Mnazimmoja, Mwanakhamis Abdallah alisema miongoni mwa sababu zinazochangia kukosekana huduma za kuridhisha katika hospitali hiyo ni msongamano wa wagonjwa kutokana na wananchi kuongezeka, uhaba wa fedha, pamoja na maslahi duni kwa wafanyakazi.
 
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akimpongeza mkandarasi wa ujenzi wa skuli ya ghorofa ya Sekondari Mpendae bwana Liu Dao Xing kutoka China, alipotembelea ujenzi huo
 
 

0 comments:

Post a Comment

 
Design by M.S Chopoti | Bloggerized by Ulimwengu Wa Digital