Vitendo vya ujambazi ni miongoni mwa vitendo vinavorudisha nyuma maendeleo mbali mbali katika jamii zetu na inapelekea mpaka watu kupotea maisha hayo yameetokeea katika mji wa Mombasa kenya baada ya washukiwa wawili wa Ujambazi kuuwawawa na umma wa watu katika eneo la Aladina Mjini mombasa Kenya
Watu wawili hao waliuwawa pale baada ya kugundulika kwa mbinu zao za kuvamia eneo hilo mnamo nyakati za magharibi kutaka kuiba zilipotibuka na kugundulika na wananchi.majambazi hao wanasadikika na miongoni mwa wale ambao walivamia nyumba moja na kuanza kuwakata kwa mapanga katika mtaa wa ganjoni mjini Mombasa wiki tatu zilizopita.
Inasemekana mmoja wa majambazi hao waliovamia nyumba hio huko Ganjoni alikuwa ni mfanya kazi wa nyumba hio na alikuwa anaijuwa vyema nyumba hio,na alipo piga hodi watu wa nyumba hawakuwa na wasi wasi kwa vile ni mtu wanayemjuwa na bila hofu wakamfungulia nyumba huku akiwa amebeba jopo la majambazi likaingia na kuanza kusahambulia
Hivyo basi katika majambazi walio uliwa wanasadikika mmoja akiwa yeye yule ambaye alikuwa mfanya kazi wa nyumba kule ganjoni.utamu wa wizi uliwanogea na malipo yake yamewafika leo kama walivyokopesha ndio walivyolipwa.na sasa miili yao imepelekwa katika Hospitali kuu ya Mkoa Coast General almaarufu Makadara.

0 comments:
Post a Comment