Marekani imesema mazungumzo kuhusu nyuklia katika mashariki ya kati yaliyopangwa kufanyika mwezi ujao hayatafanyika tena, hatua ambayo inaweza kuyakasirisha mataifa ya Kiarabu lakini ikaifurahisha Israel.
Sababu za kufutwa kwa mkutanoWizara ya mambo ya kigeni ya Marekani ilitangaza kuwa mkutano huo uliyokuwa imepangwa kufanyika katikati ya Desemba wenye lengo la kuanzisha ukanda huru dhidi ya silaha za maangamizi, na taarifa yake haikuweka wazi ni lini au kama utafanyika tena. Mwanzoni mwa mwezi huu wanadiplomasia waliliambia shirika la habari la Reuters kwamba mazungumzo hayo yalikuwa na uwezekano wa kusogezwa mbele kuliko kuyafuta kabisa.
Nuland alisema kuna tofauti kubwa miongoni mwa mataifa juu ya namna ya kushughulikia usalama wa kanda na udhibiti wa silaha, na kuongeza kuwa mataifa ya nje hayawezi kulaazimisha mchakato huo zaidi ya yanavyoweza kulaazimisha matokeo. Mpango wa mkutano wa kuweka mikakati ya uwezekano wa kuanzisha kanda isiyo na silaha za maangamizi ulikubaliwa wakati wa mkutano mwezi Mei 2010, wa wadau 189 wa mkataba wa kuzuia ueneaji wa silaha za nyuklia wa mwaka 1970, NPT.
Hofu ya Marekani
.
Wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani ilisema itaendelea kufanya kazi kujaribu kufanikisha mkutano huo, na kuongeza kuwa mkusanyiko kama huo laazima uzingatie usalama wa mataifa yote katika kanda na kuendeshwa kwa misingi ya maafikiano, na hivyo kuihakikishia Israel na wengine wote, kura ya turufu. "Hatutaki kuwa na mkutano ambapo nchi moja itashinikizwa na kutengwa," alisema Nuland, katika hatua ya wazi inayoonyesha wasi wasi wa Marekani kwamba Israel itakamiwa na washiriki wa mkutano huo
.
Matumaini bado ni madogo sana
Marekani na Israel zimesema kuwa kanda huru dhidi ya silaha za nyuklia katika kanda ya mashariki ya kati haitawezekana hadi kuwepo na amani ya kudumu baina ya mataifa ya kiarabu na Isreal, na Iran isitishe mpango wake wa nyuklia. Kama nchi za Pakistan na India zenye silaha za nyuklia, Israel haija saini mkataba wa NPT. Haikubali wala kukanusha kuwa silaha za nyuklia, ingawa wachambuzi wa uzuiaji wa kuenea silaha za nyuklia na wale wa usalama wanaamini inamiliki mamia ya silaha za atomiki
.


8:00 AM
Hamed Mazrui


0 comments:
Post a Comment