![]() |
Ukanda wa Gaza umeendelea kushambuliwa na Israeli kwa siku ya sita mfululizo, huku idadi ya waliokufa kutokana na mshambulizi hayo ikizidi kuongezea.
Jeshi la Israeli linasema kuwa limeishambulia Gaza mara 1,350 taokea siku ya Jumatano.
Mji wa Rafah kaskazini mwa Ukanda wa Gaza umekuwa ukishambuliwa katika mashambulizi ya hivi karibuni ya ndege za Israeli.
Ndege za Israeli zimeishambulia kwa makombora Wizara ya Vijana na Michezo, na uwanja wa soka wa Gaza.
Watu wawili waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mji wa Khan Yunis kusini mwa Gaza. Binti mdogo wa Kipalestina ameripotiwa kuwa katika hali mbaya.
Ripoti zinaonesha kuwa mashambulizi kadhaa ya ndege za Israeli yaliyalenga maeneo ya mashariki na magharibi mwa Gaza.
Wanawake wawili na mtoto mmoja waliuawa katika mashambulizi ya ndege ya siku ya Jumatatu mjini Gaza. Watu watatu wa familia moja nao pia waliuawa kwa mashambulizi ya ndege dhidi ya eneo la Dair al-Balah.
Wakati huo huo, makombora matatu yaliyorushwa na wapamabanaji wa Gaza yalipiga kwenye baraza la mkoa wa Eshkol la Israeli na mengine matano yakaupiga mji wa Ashkelon.
Aidha, siku ya Jumatatu, Brigedi za Izzeddin Qassam, tawi la kijeshi la Hamas, ziliishambulia kwa makombora kambi ya jeshi la Israeli ya Re’em.
Vilevile mlipuko ulisikika katika mji wa Israeli wa Eilat, ulio pembezoni mwa Bahari Nyekundu. Jeshi la Israeli lilitangaza kuwa mji huo ulipigwa na kombora kutoka palestina.
Makombora ya Gaza pia yaliipiga miji ya Be’er Sheva na Gan Yavne.
Ving'ora vya tahadhari katika miji ya Israeli ya Sha'ar HaNegev na Be'er Sheva, Bnei Shim'on na baraza la kimkoa la mji wa Eshkol vilishindwa kufanya kazi wakati wapambanaji wa Kipalestiporusha makombora yao upande wa israeli.
Televisheni ya Israeli ilitangaza kuwa mfumo wa kuzuia makombora wa Israeli unaojulikana kama Kuba la Chuma (Iron Dome) uliyakamata makombora 310 tu kati ya 1,000 yaliyorushwa na Wapalestina.
0 comments:
Post a Comment