Monday, November 26, 2012

MITIHANI KIDATO CHA PILI ZANZIBAR




 WANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI VISIWANI ZANZIBAR WAMEANZA MITIHANI YAO YA TAIFA  KATIKA SHULE MBALI MBALI ZA MJINI NA MASHAMBA.

KATIKA HALI ISIYOTARAJIWA WANAFUNZI WENGI WALIONEKANA KULALA KATIKA VYUMBA VYA MITIHANI WAKATI MITIHANI HIYO IKIENDELEA.

SOMO LA HESABU NDIO LILIKUA SOMO LA UFUNGUZI KATIKA MITIHANI HIYO..AMBAPO WATAHINIWA WENGI WALIONEKANA KUTOKA MAPEMA KATIKA VYUMBA VYA MITIHANI HALI AMBAYO ILIWAPA WASI WASI MKUBWA WASIMAMIZI WA MITIHANI HIYO.

MITIHANI HIYO IMEANZA SAA MBILI KAMILI ASUBUHI  HADI SAA NANE KAMILI MCHANA AMBAPO KILA SIKU WATAFANYA MITIHANI MIWILI MIWILI.

WAKIZUNGUMZIA HALI HALISI YA MITIHANI HIYO BAADHI YA WANANFUNZI KWA NIABA YA WENZIWAO WAMESEMA MPAKA SASA HALI YA MITIHANI INAKWENDA VIZURI NA HAKUNA TUKIO LOLOTE LA UDANGANYIFU LILOJITOKEZA KATIKA BAADHI YA SKULI TULIZOTEMBELEA ZA WILAYA YA MJINI MAGHARIB.  ZIKIWEMO JANGOMBE, HAILESELASIE, MWEMBELADU, MWANAKWEREKWE NA FUONI,  

 AIDHA WAMEWATAKA WANAFUNZI WENZAO KUJIAMINI NA KUONGEZA JUHUDI ILI KUWEZA KUFAULU KWA WINGI KATIKA MTIHANI YAO .
VILE VILE WAMEWAOMBA WASIMAMIZI WAO KUWA WAADILIFU NA KUTUMIA BUSARA KATIKA USIMAMIAJI WAO  ILI KUWEZA KUONDOA HOFU KWA WANAFUNZI.

NAO KWA UPANDE WA WASIMAMIZI WA MITIHANI HIYO WAMESEMA IPO HAJA KUBWA SANA YA WAZAZI KUSHIRIKIANA NA WALIMU ILI KUWEZA KUWAJENGEA MUSTAKABALI MZURI WANAFUNZI. KWANI IMEONEKANA WANAFUNZI  WENGI HAWANA TAALUMA ZA KUTOSHA,

MITIHANI HIYO IMEANZA LEO KWA SOMO LA HISABATI NA HISTORIA NA KUTARAJIWA KUMALIZIKA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 2-12-2012.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by M.S Chopoti | Bloggerized by Ulimwengu Wa Digital