Mtoto wa ajabu mwenye jinsia ya kike amezaliwa jana katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro huku viungo vyake vya ndani ya mwili vikiwamo utumbo, figo, maini na bandama vikiwa nje, muuguzi katika wadi ya kina mama wajazito, Mercy Matogo, amesema kuwa nikweli walimpokea mama wa mtoto huyo, Hadija Issa, majira ya asubuhi akiwa ana maumivu ya uchungu wa kujifungua, na walimpatia huduma katika hospitali hio hadi majira ya saa sita mchana mwenyezinmungu akamfanikisha kujifungua motto huyo wa ajabu
Amesema wakati mama huyo akijifungua, wao walishangaa kuona motto motto huyo aliezaliwa kutanguliza vitu vya ndani ya tumbo tofauti na hali ya kawaida kwa binadamu wengine ambao huzaliwa kwani ni kawaida kwa motto anapozaliwa kutanguliza kichwa wakati wa kuzaliwa,madaktari wa hospitali hio wamesema mara tu baada ya kumto mtoto huyo walibaini kuwa viungo vyote vya ndani vya motto huyo vilikuwa vipo nje .
Aidha mwili wa motto huyo haukuwa na kitovu wala sehemu ya haja kubwa wala haja ndogo lakini watalamu baada ya kumchunguza walibaini kuwa motto huyo alikuwa na jinsia ya kike,lakini cha kusikitisha zaidi ni kwamba motto huyo alifariki baada ya muda mdogo wa kuzaliwa kwake.
Kwa upande wake afisa mkuu wa wadi hiyo, Santieli Kinyingo, alisema tukio hilo ni geni katika wadi hiyo pia amsema tukio hilo linaweza kutokana na sababu mbali mbali ikisibitisha miongoni mwa sababu zinazoweza kusababisha hilo ni mjamzito kutumia dawa za kienyeji au ya kisasa bila ya kupata ushauri kutoka kwa daktari.
Kwa upande wake mama motto huyo Bi Khadija Issa anmbae ni mkaazi wa msamvu mjini Morogoro amesema kuwa mamba hiyo ilikuwa ni yakwanza kwake na hakuwahi kuona dalilin zozote mbaya wakati wa ujauzito wake hivo basi amesikitishwa sana nna tukio lililomtokea.


11:59 PM
Hamed Mazrui


0 comments:
Post a Comment