Mwalimu wa Shule ya Msingi Kwamwachalima, iliyopo katika Kijiji cha Kwamwachalima Kata ya Komkonga wilayani Handeni Mkoa wa Tanga, ametoweka baada ya kutuhumiwa kufanya mauaji ya kinyama kwa mwanafunzi wa darasa la tatu na kumjeruhi vibaya mwingine wa kidato cha pili.
Mwalimu huyo, Suhalungi Nangoma (23) anatafutwa na Polisi kwa tuhuma hizo
za kuua pamoja na kujeruhi kwa kisu wanafunzi hao ambao ni ndugu, na ni watoto wa mwalimu mwenzake, Ijumaa Mjaliwa wanaefundisha pamoja skulini hapo.
.
Nangoma anatuhumiwa kumuua kwa kumchoma kisu kifuani binti huyo anayesoma darasa la tatu katika shule hiyo, Farihia Mjaliwa (9), kisha kumjeruhi kwa kumcharanga kisu tumboni kaka wa binti huyo, Mohamed Farhia anayesoma kidato cha pili katika Sekondari Kisaza

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Jafari Mohamed alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema polisi wanaendelea kumsaka mtuhumiwa ili afikishwe mahakamani.
0 comments:
Post a Comment