Tuesday, November 27, 2012

Shamhuna aitolea uvivu wizara ya elimu Tanzania bara

Waziri wa Elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Mh Ali Juma Shamhuna  ameilaumu wizara ya elimu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania bara  kwa madai ya kutoishirikisha Zanzibar ipasavyo katika mabadiliko mbali mbali hususani katika suala la mitihani ya Taifa

Ameyasema hayo mbele ya makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad huko makao makuu ya wizara hiyo mazizini, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara ya makamo wa kwanza wa rais katika sekta ya elimu.
Aidha mh Shamhuna amesema kuwa wizara ya elimu tanzania kupitia baraza la mitihani la taifa, mara nyingi imekuwa ikafanya maamuzi bila ya kuishirikisha wizara ya elimu zanzibar, jambo ambalo linawapa ugumu wa kuetekeleza mipango yao ikiwa ni pamoja na kuwaandaa wanafunzi kuweza kuyafahamu mabadiliko yanayofanywa na baraza la mitihani na ni miongoni mwa mambo yanayowapelekea wanafunzi wa zanzibar kutokufaulu mitihani ya taifa.
Kwa upande wake makamu wa kwanza wa rais Maalim Seif amezishauri wizara hizo kukaa pamoja na kujadiliana kuhusu hatua bora za kuchukuliwa katika kuondosha tofauti hizo, na kuelezea haja ya kuwepo kwa mashirikiano ya karibu kati ya wizara hizo mbili.

Baada ya kupokea taarifa ya wizara hiyo iliyowasilishwa na naibu katibu mkuu bw. Abdalla mzee, maalim seif alihoji uhaba wa madarasa ya kusomea pamoja na vikalio katika skuli mbali mbali unguja na pemba.
Aidha maalim seif ameelezea haja ya kurejeshwa kwa huduma za dakhalia ili kuwaondoshea usumbufu wanafunzi wanaotoka maeneo ya mbali, hoja ambayo imeungwa mkono na uongozi wa wizara hiyo kwamba wamelifikiria kwa muda mrefu suala hilo licha ya kukabiliwa na ufinyu wa 
 
Hamed Mazrui added a new photo.
Photo
 
 

0 comments:

Post a Comment

 
Design by M.S Chopoti | Bloggerized by Ulimwengu Wa Digital