Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Ahmad Kilima
MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), itasitisha utoaji wa leseni mpya za usafirishaji wa abiria katika Jiji la Dar es Salaam kwa mmiliki mmoja mmoja kuanzia Desemba Mosi mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Sumatra, Ahmad Kilima, ilisema hatua hiyo inatokana na kushauriana kati ya Sumatra, na wamiliki wa Daladala, Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi (Dart) na wadau wengine.
Wakati wa mkutano wa kukusanya maoni uliofanyika mwanzoni mwa mwaka 2010 ,baadhi ya wamiliki wa daladala walipinga utaratibu huo kutokana na uwezo wao kifedha kuwa mdogo wakihofia kuwa kuwaathiriAidha alisema kuwa katika kipindi cha kuanzia Desemba mosi mwaka huu hadi Juni 30 mwaka kesho, wasafirishaji wanaotoa huduma katika njia hizo, wanashauriwa kujiunga na kuanzisha makampuni au ushirika ili waweze kupewa leseni za kutoa huduma kuanzia Julai Mosi mwaka kesho,” alisema.
i.
0 comments:
Post a Comment