Monday, November 26, 2012

tulikubaliana mafuta zanzibar kuwa mali ya muungano waziri mkuu mstafu asema

Wakat, hule mimi nilipokuwa Waziri Mkuuwa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania niliongoza ujumbe wa Serikali ya Muungano na Marehemu Dr Omar aliekuwa Waziri Kiongozi aliongoza ujumbe wa Serikali ya Zanzibar tukazungumza na kukubaliana kuwa mafuta yaliokuwepo Zanzibar yawe ni mali ya Muungano leo hii nashangaa wanatokea baadhi ya watu kwa kusema kuwa mafuta ni ya Zanzibar na si yamuungano.

Kihistoria hapo zamani Waarabu ndio waliokataa Muungano lakini Afro Shirazi wale wenzetu walikubali Muungano,na tukaungana kwania safi na wenzetu inawezekana hawa waarabu walioukataa mungano kipindi kile kwa sasa ndio wanaochochea kuvunjika kwa Muungano kule Zanzibar kama vile treni ya zamani inavyochochewa moto.
Hayo yamesemwa na aliekuwa waziri mkuu mstaafu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mzee - John Malesela wakati alipokuwa akifanya mahojiano na kituo cha itv

0 comments:

Post a Comment

 
Design by M.S Chopoti | Bloggerized by Ulimwengu Wa Digital