Sunday, November 25, 2012

Vietnam kusadia mipango ya uchumi Zanzibar


Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein ametaka Zanzibar na Vietnam kushirikiana katika sekta za uvuvi, utalii, kilimo na biashara.
Aliyataja kuwa ni miongoni mwa maeneo muhimu ya kuimarisha ushirikiano kati Zanzibar na Vietnam katika kufanikisha mpango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) wa kukuza uchumi na kupunguza umasikini (MKUZA).
Rais aliyasema hayo akiwa nchini Vietnam ambapo alikutana na Makamu wa Rais wa nchi hiyo Nguyen Thi Doan huko Ikulu mjini Hanoi na taarifa yake kupatikana jana mjini Zanzibar.
Dk. Shein alimueleza mwenyeji wake kuwa serikali imeamua kuimarisha sekta hizo muhimu kiuchumi ambazo kuna haja ya mataifa hayo kushirikiana katika kuziendeleza.
Alisema Tanzania na Vietnam zimekuwa na uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu kuanzia miaka ya 1960 na zimeweza kuungana mkono katika mambo mbali mbali ya kimaendeleo, kiuchumi na hata kisiasa.
Dk. Shein alimueleza kingozi huyo hatua zinazochukuliiwa na SMZ katika kuimarisha sekta za maendeleo na uchumi na mafanikio yaliofikiwa katika kutekeleza Dira ya 2020 pamoja na MKUZA.
Dk Shein alisema Tanzania imeweka mpango kazi maalum wa kuimarisha maeneo hayo ya kiuchumi ambapo sekta ya kilimo imepewa kipambele kikubwa kutokana na sekta hiyo kuwa nguzo ya uchumi wa Zanzibar.
Alisema Zanzibar imeamua kufanya mapinduzi ya kilimo cha kisasa ikiwemon cha umwagiliaji pamoja na kuweka mpango maalum wa kuwapatia ruzuku ya pembejeo wakulima.
Aliongeza kuwa chini ya mpango huo wa mapinduzi ya kilimo cha kisasa serikali imeamua kuimarisha Chuo cha Utafiti wa Kilimo Kizimbani na kusisitiza haja ya kuwepo mashirikiano katika mambo ya utafiti ili kuongeza uzalishaji kupitia sekta ya kilimo visiwani Zanzibar.
Kuhusu sekta ya utalii Rais wa Zanzibara alisema kwamba serikali inaendelea na utekelezaji wa sera ya utalii kwa wote kutokana na sekta hiyo kuonyesha mafanikio makubwa kwa kuchagia asilimia 25 ya pato la taifa na asilimia 83 ya fedha za kigeni zinazokusanywa kila mwaka.
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa VietnamDoan, alitoa pongezi kwa Dk Shein kwa kukubali mwaliko wa nchi hiyo kwa ajili ya ziara hiyo hatua ambayo inaonyesha wazi jinsi Zazibar inavyothamini uhusiano na ushirikiano kati ya mataifa haya.
Aliahidi kuwa Vietnam itaendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuimarisha sekta mbali mbali za maendeleo ikiwemo miradi ya kilimo , utalii na uvuvi.
“Tuko tayari kufanya mazungumzo ya kuwakutanisha viongozi wa Zanzibar wakiwemo Mawaziri na wenzao wa Vetnam kuangalia maeneo ya kushirikiana katika kukuza sekta za maendeleo, “ alisema kiongozi huyo
.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

0 comments:

Post a Comment

 
Design by M.S Chopoti | Bloggerized by Ulimwengu Wa Digital