Wednesday, November 21, 2012

Waziri wa Michezo Said Mbaruok, Aikibidhi bendera Zanzibar Heroes Bwawani.

 Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk (kushoto)akimkabidhi Bendera Nahodha wa timu ya  Taifa ya Zanzibar Heroes, Nadir Haroub Kanavaro, akishuhudia Makamu Mwenyekiti wa ZFATaifa Alhaj Haji Ameir.makabidhiano hayo yamefanyika katika katika ukumbi wa hoteli ya bwawani Zanzibar katika makabidhiano hayo waziri huyo amewataka wachezaji hao wa timu ya taifa zanzibar kuweka mbnele utaifa wao kwa lengo la kuitetea nchi yao katika mashindano ya kombe la chalengo yatakayoanza hivi karibuni huko nchini uganda
 
Amesema kuwa iwapo timu hio ya zanzibar itaweza kutwa kombe hilo kutaweza kuijengea sifa sana nchi yetu katika nyanja mbali mbali duniani hivo basi amewataka wachezaji hao kujituma kwa ari ili waweze kurudi na kombe hilo nyumbani mwaka huo kitu ambacho hata rais wa zanzibar Dr Ali Mohd Shein amesistiza kuwa mara hii atafarijika kuona kombe hilo linaletwa Zanzibar.
 
Kwa upande wake kapteni wa timu hio Nadir Haroub Kanavaro ambae ni beki mahiri wa timu ya yanga ya daresalam amemuhakikishia waziri huyo kuwa timunhio itajituma ena kwa ari yote ili kuhakikisha wanalileta ko,be jilo visiwani Zanzibar

0 comments:

Post a Comment

 
Design by M.S Chopoti | Bloggerized by Ulimwengu Wa Digital