Thursday, November 29, 2012

yaliojiri mahakama ku vuga dhidi ya viongozi wa uamsho leo hii


kufuatia kesi inayowakabili viongozi wa jumua ya uamsho kisiwani Zanzibar ilioendelea leo hii katika mahaka kuu vuga baada ya mawakili wa viongozi hao kulalamikia kuwepo kwa Jaji asieweza kutoa dhamana kwa watuhumiwa hao ndani ya kesi yao hivo basi mawakili hao waliwasilisha madai yao mahakamani hapo  ya kubadilishiwa jaji katika kesi inayowakabili viongozi hao wa jumuia a uamsho ambapo jaji atakaeisikiliza kesi hio awe na uwezo wakutoa maamuzi na sio kuendeshwa na jaji asiekuwa na uwezo wa kuiamulia kesi hio.
kutokana na maombi ya mawakili hao  dhidi ya wateja wao leo hii  wamefanikiwa kuweza kubadilishiwa jaji ambae atakuwa na uwezo kwa kuitolea maamuzi kesi hio na tayari ameanza kuisikiliza kesi inayowakabili watuhumiwa hao kwa kuanza kuwataja majina yao tu na badae kesi hio kuahirishwa hadi tarehe sita mwezi unaofata.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by M.S Chopoti | Bloggerized by Ulimwengu Wa Digital