Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed shein, na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,wakipokea mashada ya mauwa kama ni Ishara ya ukaribisho katika Ikulu ya Vietnam,alipofika kwa mazungumzo na Makamo wa Rais wa Vietnam Bibi, Nguyen Thi Doan,akiwa na ujumbe wake katika ziara rasmi ya Kiserikali nchini humo ya wiki moja.[Picha na Ramadhan Othman Vietnam.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed shein, akisalimiana na Mawaziri na Viongozi mbali mbali wa Nchini Vietnam ,alipofika ikulu ya nchi hiyo kwa mazungumzo na Makamo wa Rais Vietnam Bibi, Nguyen Thi Doan, akiwa katika ziara rasmi ya Kiserikali nchini humo ya wiki moja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed shein, akiwatambulisha Viongozi aliofuatana nao kwa Makamo wa Rais wa Vietnam Bibi,Nguyen Thi Doan,walipowasili Ikulu ya nchi hiyo kwa mazungumzo,ya kuimarisha uhusiano na Ushirikiano baina ya pande zote, akiwa katika ziara rasmi ya wiki moja nchini humo.
Viongozi wa Serikali waliofuatana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wakiwa kwenye mkutano maalum na uongozi wa serikali ya Vietnam.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed shein,(katikati) akiwa ujumbe aliofuatana nao katika Mkutano maalum na Uongozi wa Serikali ya Vietnam,ukiongozwa na Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Bibi Nguyen Thi Doan,(hawapo pichani) katika ukumbi wa Ikulu ,katika kuimarisha Uhusiano na Ushirikiano baina ya pande mbili hizo,katika ziara rasmi ya Kiserikali.
Thursday, November 22, 2012
Dk.Shein Awasili Nchini Vietnam Leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Maofisa wa Serikali ya Vietnam, alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hanoi Nchini Vietnam, akiwa katika ziara rasmi ya Kiserikali


2:48 AM
Hamed Mazrui







0 comments:
Post a Comment