Thursday, December 13, 2012

JAMII IMETAKIWA KUKIMBILIA SEHEMU HUSIKA PALE INAPOPATWA NA MATATIZO



Jamii kwa ujumla imetakiwa kuhakikisha kuwa inakimbilia sehemu husika pale wanapopatwa na matatizo na sio kubaki majumbani tu wakidhani ndio suluhisho la matatizo yao hayo yamesemwa na mkuu wa kitengo cha kudhibi na kukinga maradhi yanayotokana na maambukizo Zanzibar  ( epidemiology) Dr Salma Masauni alipokuwa akitoa ufafanuzi kufuatika kifo cha mtoto kilichosababishwa na mbwa kichaa.


Mtoto Jaha Wajibu Makame mwenye umri wa miaka kumi amefariki dunia  huko katika kijiji cha Ndijani kongo,kutokana na  kutafunwa na mbwa asiejuulikana mwenyewe kijijini hapo na kumsababishia maumivu makali lakini kutokana na   msaada wa Baba wa mtoto huyo Bwana Wajibu makame aliweza kumpatia huduma mtoto wake huyo kwa kumpaka spirit na ndimu ambapo aliweza kuyapunguza maumivu makali aliokuwa nayo mtoto  wake huyo.

Hatuwa iliofanywa na Mzazi huyo iliweza kumfanya mototo huyo kupona kabisa kidonda alichokuwa nacho na hatimae kuweza kuendelea na shughuli zake kama kawaida,lakini  baada ya miezi mine hali ilibadilika kwa mtoto huyo alianza kupata maumivu katika maeneo aliotafunwa na wazazi wake kuamua kumfikisha katika hospitali ya Ndijani mseweni kwa ajili ya matibabu.

 Kufuatia tatizo alilokuwa nalo mtoto huyo madaktari wa hospitali hio kwa kushirikiana na afisa wa utafiti juu ya maradhi wilayani humo Dr Sleima Saleh pamoja pamoja na maafisa kutoka katika kitengo cha kudhibiti na kukinga maradhi yanayotokana na maambukizi waliwezesha kumfikisha motto huyo katika hospitali kuu ya mnazi mmoja kwa matibabu zaidi.

Mara tuu baada ya kufikishwa katika hospitali hio siku ya Alhamis tarehe 6 mwezi wa 12  aliweza kupatiwa matibabu ya haraka kwa kuchomwa sindano ambayo inaonekana ilimsaidia tu kwakuondoa maumivu lakini haikuweza kuondoa tatizo hilo kutokana na kukaa muda mrefu bila ya kupatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa wa wahusika kutoka kitengo cha kukinga na kudhibidi maradhi ya maambukizi Zanzibar  wamesema kuwa mtoto huyo aliweza pia kumtafuna Mamake mzazi wakiwa hospitalini hapo lakini kwa bahati nzuri akiweza kupatiwa matibabu ya haraka, na hadi jana mnamo tarehe 12 /12 majira ya asubuhi mtoto huyo alifariki dunia.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by M.S Chopoti | Bloggerized by Ulimwengu Wa Digital