Thursday, December 13, 2012

JESHI LAPOLISI LAIMARISHA ZAIDI ULINZI MKALI UWANJA WA GOMBANI



                 

 

Ligi daraja la Pili Taifa Pemba, limeendelea kurindima tena katika kiwanja cha Gombani kisiwani Pemba, chini ya ulinzi mkali wa Askari polisi, kwa kuikutanisha timu ya Shaba na Umeme kutoka kiuyuminungwini, ambapo juzi pambano kati ya Timu ya Stone Town na Shaba limeshindwa kufanyika kufuatia kutokuwepo kwa ulinzi kiwanjani hapo

Katika pambano hilo timu ya Shaba kutoka maeneo ya kisiwa kidogo cha Kojani, waliweza kuwavitisha nanga watani wao wa jadi kutoka Kiuyuminungwini timu ya umeme kwa kuitandika goli 3-1.

Mchezo huo uliokuwa mgumu kwa timu zote, kutokana na timu hizo kila zinapokutana, shaba ilijipatia magoli yake matatu kupitia kwa wachezaji wake Suleiman Issa dakika 14 na 89 na Bakari Suleiman dakika 48, huku goli pekee la Umeme likifungwa na Moh’d Abdallah.

Nayo Sharp Victer ikaitandika timu ya Diver ya makoongwe goli 2-0, Maji Maji wakatandikwa goli 2-0 na timu ya Imara, Rambo ikakubali kipigo cha goli 2-1 kutoka kwa Dogomoro,

Nao walalamikaji wa kudumu katika ligi hiyo, ama Shaba B, timu ya Buyuni ambayo imepatiwa jina hilo na mashabiki wasoka katika kiwanja cha Gombani, wamelazimishwa sare ya goli 2-2 na timu ya Read Ster.

Kwa matokeo hayo kundi “A”limeendelea kukabana koo katika kugombani nafasi ya kwanza ili kuongoza kundi hilo. Ambapo Uwandani inaongoza kundi hilo ikiwa na alama 22, Sharp Victer yapili ikiwa na alama 20, Okapi na Kidike zote zikiwa na alama 19 tafaouti ya magoli ya kufungwa na kufunga , Kundi “B” linaongozwa na Maji Maji na Small Renger zote zikiwa na alama 19, Black Wizard ikiwa na alama 18 ikifuatiwa na Chuoni alama 15



 NA ABDI SULEIMAN,PEMBA.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by M.S Chopoti | Bloggerized by Ulimwengu Wa Digital