Thursday, December 6, 2012

Kilichoendelea mahakama kuu jana dhidi ya viongozi wa uamsho.

Jeshi la Polisi likidumisha ulinzi katika mahakama kuu vuga wakati wakusikilizwa kesi ya viongozi wa uamsho.Viongozi hao wa jumuia ya uamsho ambao ni watuhumiwa  walifikishwa mahakamani hapo majira ya saa tatu za asubuhi wakiwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi pamoja na JKU wakiambatana na KKM na hakuweza kuruhusiwa mtu yoyote kupita njia iliokuwa ikielekea mahakama kuu kutokana na jeshi hilo kuhofia wananchi kufanya vitendo visivotakiwa mahakamani hapo, na kuhusu suala laraia kuweza kufatilia kesi hio hawakuweza kuruhusiwa isipokuwa ni watu wawili tu walioruhusiwa kuingia tena kwa mujibu walivosema wenyewe nikwamba waliomba dua sana na walifika mapema hapo mahakamani.
Kesi iliosikilizwa leo ni kuhusu madai yao ya msingi waliowasilisha mawakili wao kuwa watuhumiwa wao kunyimwa haki za msingi wawapo gerezani kwani wateja wao wamekuwa hawatendewi haki wanapokuwa humo wananyimwa kula kutoka majumbani kwao pia mawakili wamesema wateja wao hawatendewi haki kwani wamekuwa wakiwekwa kila mtu na chumba chake hali ambayo si sheria kabisa pamoja na kukosa huduma muhimu wanapokuwa huko,
Lakini kwa sasawatuhumiwa hao tayari wameanza kutekelezewa baadhi ya huduma huzo kwani tayri wameweza kuchanganywa na watu wengine waliomo ndani ya gereza hilo,pia wameruhusiwa kuletewa chakula lakini sio kuletewa na jamaa zao bali jumua wenyewe ndio wawaletee.
Na kuhusu suala la kesi zinazowakabili viongozi hao wa uamsho bado haisikilizwa kabisa kutokana na ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka kutokukamilisha upepelezi wa kesi hizo zinazowakabili watuhumiwa hao hivo basi mahakama imeamuru watuhumiwa hao kurudishwa rumande hadi tarehe 19 mwezi huu.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by M.S Chopoti | Bloggerized by Ulimwengu Wa Digital