Thursday, December 13, 2012

KUWA KUWEPO KWA UWAZI NA UWAJIBIKAJI KWA WATENDAJI NA WADAU WA SEKTA ZA KIJAMII KUTASAIDIA KUHARAKISHA HARAKATI ZA UTEKELEZAJI KATIKA MIPANGO YA MAENDELEO

IMEELEZWA KUWA KUWEPO KWA UWAZI NA UWAJIBIKAJI KWA WATENDAJI NA WADAU WA SEKTA ZA KIJAMII KUTASAIDIA KUHARAKISHA HARAKATI ZA UTEKELEZAJI KATIKA MIPANGO YA MAENDELEO YA TAIFA  ILI KUPUNGUZA UMASIKINI KWA WANANCHI WENYE KIPATO CHA CHINI.
 
 AKIZUNGUMZA KATIKA UFUNGAJI WA SEMINA YA SIKU MBILI MWEZESHAJI KUTOKA AFISI YA MAKAMO WA PILI WA RAIS DR.ABUBAKAR RAJAB  KATIKA KUJADILI MKAKATI WA MAWASILIANO WA MPANGO WA KUPUNGUZA UMASIKINI ZANZIBAR MKUZA II  HUKO KATIKA UKUMBI WA HOTELI YA BWAWANI.
 
 AMESEMA KUWA TATIZO LA UMASIKI LINAATHIRI MIKAKATI MBALIMBALI YA MAENDELEO HASA KATIKA NYANJA ZA KIJAMII,KIUCHUMI NA KITAMADUNI HIVYO NI MUHIMU KUWEPO UTEKELEZAJI WA MIPANGO YA MAENDELEO KWA VITENDO.
            DR.ABUBAKAR AMEFAHAMISHA KUWA WATENDAJI WANATAKIWA KUFANYA KAZI YA ZIADA KWA KUTOA TAARIFA SAHIHI JUU YA UTEKELEZAJI WA MIPANGO YA MAENDELEO ILI ZIWAFIKIE KWA WAKATI WANANCHI WA VIJIJINI.
 
AIDHA AMESEMA MKUZA II INA MALENGO YA KUIMARISHA HUDUMA MUHIMU ZA KIJAMII  KWA LENGO LA KUPUNGUZA UMASIKINI ILI KUFIKIA MALENGO YA MILENIA.
 
NAO WASHIRIKI KATIKA MAFUNZO HAYO WAMESEMA TAALUMA WALIYOIPATA ITASAIDIA KUTOA ELIMU KWA JAMII ILI KULETA MABADILIKO JUU YA UELEWA WA MIPANGO YA MAENDELEO HUSUSANI MKUZA II.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by M.S Chopoti | Bloggerized by Ulimwengu Wa Digital