Tuesday, December 4, 2012

Maalim Seif aipongeza Zanzibar Heroes

Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad
Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ametuma salamu za pongezi kwa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kwa kufanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali kwenye michuano ya kombe la challenge. Zanzibar Heroes imeingia hatua hiyo baada ya kuifunga timu ya Burundi kwa mikwaju ya penalti (6-5) kwenye uwanja wa Lugogo mjini Kampala, Uganda kufuatia timu hizo kutoka sare ya bila kufungana katika dakika zote 90 za mchezo.
Katika salamu hizo Maalim Seif alisema Zanzibar Heroes wanaendelea kudhihirisha uwezo wa Zanizbar wa kuweza kushiriki katika mashindano ya kimataifa.
Ameitaka timu ya Zanzibar Heroes kuongeza juhudi katika mchezo wake wa nusu fainali ili kuendeleza ushindi wake na hatimaye kuweza kutwaa Kombe hilo la Challenge katika msimu huu.

Na Hassan Hamad OMKR

0 comments:

Post a Comment

 
Design by M.S Chopoti | Bloggerized by Ulimwengu Wa Digital