Wakuu kadhaa wa serikali na mawaziri wamewasili Doha, Qatar kwa ajili ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira, mkutano ambao umegubikwa na mabishano juu ya fedha na ahadi zinazotakiwa kuzuia gesi chafu.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon anatarajiwa kuhutubia mkutano huo wa washiriki zaidi ya 11,000 majira ya saa 9 kwa saa za Afrika mashariki, na anatarajiwa kuhimiza mataifa kuweka pembeni tofauti zao kwa ajili ya mustakabali ya sayari ya dunia.Hata baada ya kutolewa kwa tahadhari juu ya hatari inayoikabili dunia kutokana na gesi chagu, wangalizi wanasema karibu mataifa 200 yanayoshiriki mazungumzo ya Doha yemeendelea kugawanyika juu ya masuala muhimu kwa ajili ya kufukia makubaliano kuhusu mabadiliko ya tabianchi.
Shabaha ya Umoja wa Mataifa
Maazimio kuhusu masuali yote mawili kabla ya kumalizika kwa mkutano huo siku ya Ijumaa yatasafisha njia ya kuwepo na mkataba mpya na mpana ambao unatakiwa usainiwe kabla ya mwaka 2015 na kuanzwa kutekelezwa mwaka 2020 ili kupunguza joto la dunia.
Shabaha ya Umoja wa Mataifa ni kupunguza kiwango cha joto la dunia kufikia nyuzi joto mbili, ambazo wanasayansi wanasema zinaweza kusisadia dunia kuepekua athari mbaya zaidi za mabadiliko ya tabia nchi.
Mkuu wa Tabia Nchi wa Umoja wa Mataifa, Christiana Figueres, ameelezea kusikitishwa kwake siku ya Jumatatu, kuhusiana na kasi ndogo ya mazungumzo hayo, wakati baadi ya wajumbe wakionyesha hofu ya mkwamo kabla ya kuwasili kwa mawaziri kutoa msukumo wa mwisho wa kisiasa.


11:52 PM
Hamed Mazrui


0 comments:
Post a Comment