Saturday, December 15, 2012

WADAU KISIWANI PEMBA WAPENDEKEZA KUANZISHWA KWA MAHAKAMA YA WANYAMA




WADAU wa kusimamia haki za wanyama,wamependekeza kuanzishwa kwa Mahakama maalum itakayosikiliza kesi za ukatili wa wanyama, ili kupunguza ukatili huo uliokithiri kwa wafugaji na watumiaji wengine.

Walisema katika siku za hivi karibuni kumejitokeza kwa kiwago kikubwa cha  ukatili dhidi ya wanyama na ndege, bila ya watendaji wa ukatili huo kujali wakijua kuwa hakuna adhabu itayowakumba

Wadau hao walieleza hayo jana huko ukumbi wa Magofu Chake chake wakati walipokuwa wakichangia marekebisho ya sheria namba 11 ya mwaka 1999 ya kuwalinda wanyama ilipowasilishwa na wanasheria kutoka Tume ya marekebisho ya sheria kupitia Wizara ya Katiba na Sheria.

Walieleza kuwa vitendo hivyo vimekuwa vikichangiwa na kutokuwepo kwa Mahakama maalum za kushughulikia kesi za ukatili na udahililishaji wa wanyama, hivyo kama Wizara husika itanzisha mahakama hiyo, vitendo hivyo vinaweza kupungua kwa kasi.

Mgeni Said Mgeni kutoka kituo cha Polisi Chake chake, alisema pamoja kwamba kwa baadhi ya wakati kesi mbali mbali hucheleweshwa kuanzia Jeshi la Polisi , Mahakamani na jamii yenyewe, lakini kuwepo kwa Mahakama ya wanyama itasaidia.

Alifafanua kuwa wamiliki wa wanyama kama vile Punda na Ng’ombe wamekuwa mstari wa mbele kutumikisha bila ya kiasi kwa kupakiwa mizigo mizito bila ya kupewa muda maalum wa kupunzika.

‘’Wenye gari za Ng’ombe na Punda wamekuwa wakiwapakia wanyama wao mizigo mingi na bakora juu, na anapita mbele ya vyombo vya sheria, lakini sheria dhaifu na kutokuwepo kwa mahakama ya wanyama kumechangia kuendelea’’.alifafanua.

Nae sheha wa Shehia ya Ndagoni Massoud Ali Mohamed alisema uhaba wa madaktari wa wanyama kwa baadhi ya wakati, huchangia kuingizwa kwa wanyama kutoka nje ya Kisiwa cha Pemba bila ya kuchuungzwa.

Alieleza kuwa wakati mwengine wanyama hao wamkuwa na maradhi lakini hata wanapowakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria, hakuna hatua yoyote inayochukuliwa.

Mapema wakiwasilisha sheria hiyo na historia yake, mwanasheria kutoka Tume ya Marekebisho ya sheria Ali Mohamed, alisema sheria hiyo baadhi ya vifungu haviendani na wakati uliopo ikiwa ni pamoja adhabu ndogo kwa mkatili wa wanyama.

Nae mwanasheria Khamis Mwita wakati akiwasilisha maoni ya sheria hiyo namba 11 ya mwaka 1999 kutoka kwa wanasheria alisema, wamebaini kuna vipengele kadhaa ambavyo havikidhi haja kwa wakati huu

 Na Haji Nassor, Pemba

0 comments:

Post a Comment

 
Design by M.S Chopoti | Bloggerized by Ulimwengu Wa Digital