Saturday, December 15, 2012

WAJASIRIAMALI KISIWANI PEMBA WAITAJI KUENDELEZWA KITAALAMU

               
WARATIBU wa Mradi wa Ujasiriamali na Maisha kwa wanawake wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wamesema ipo haja ya kuendelezwa kitaaaluma kwa malengo ya kufanikisha azima zao mbali mbali zikiwemo zile za kuweza kugombea nafasi mbali mbali za uongozi.
 
Walisema pindipo watakuwa wakipata fursa za kuweza kuwezeshwa  watakuwa ni wenye kupiga hatua kubwa katika  kuendeleza na kupanga mikakati ya kufanikisha malengo hayo.
 
Hayo wameeleza wakati walipokuwa wakichangia mada ya ungozi kwa mwanamke na mada ya haki za binaadamu katika semina iliyofanyika katika ukumbi wa weni Wilaya ya Wete.
 
Walisema jitihada za WEZA pekee ndio zilizowafikisha akinamama kuweza kutoka katika hali waliyokuwa nao  na  sasa akinamama hao kuweza kubadilika  na kupata maendeleo .
 
Mmoja kati ya Waratibu hao Khadija Mohammed Said wa shehia ya Chwale   alisema changamoto zipo nyingi katika jamii na  hasa suala la kukosa elimu kwani ndio chanzo cha  changamoto hizo.
 
Alifafanuwa kuwa jamii inataka kuweza kubadilishwa  katika mambo yote ikiwa ni pamoja na kushawishiwa  katika kufanya mambo ya meendeleo.
 
Naye Riziki Abdalla Kombo wa Shehia ya Mjananza Wilaya ya Wete alisema  ingawa wajanajamii wanabadilika kidogo kidogo  ila ipo haja ya kuwaelimisha ili nawa wao waweze kujitetea na kuweza kusimama na kugombea  nafasi mbali mbali katika uongozi.
 
“Tunataka tugombee ila wanajamii wezetu wanaturudisha nyuma ila kupata semnina  hii imekuwa  ni moja ya kuweza kujielewa na kuweza kujipanga na kusimama na tukaweza kugombea”alisema Riziki .
 
Walisema wataribu hao kuwa wamezidi kuelewa  sifa na vipi mwanamke ambaye anahitaji kugombea katika nafasi mbali mbali moja ik,iwa ni kuweza kuwa na mashirikiano na wezake,awe ni mtu mwenye busara na mwenye kukubalika katika jamii.
 
“Mtu lazima awe muajibikaji ndipo atakapofanya kazi zake kwa uwajibaki bila ya kuweza kusimamiwa”walisema.
 
Aidha mshereheshaji katika semiana hiyo Hassan Abdalla Rashid kutoka Katiba na Sheria  alisema mafunzo hayo yatawewezesha wanawake hao kujirtathmini na kuweza kujuwa ni vipi waweze kushiriki katika mambo mbali mbali ikiwemo la uongozi huku ikiwa ni watu wenye kujiaamini na kujuwa lipi wanalofanya.
 
Hata hivyo naye Afisa Uwezeshaji kutoka katika mradi wa ujasiriamali Pemba Jitihada Abdalla amesema lengo la semina hiyo ni kuwajengea uwezo wanawake katika kuelewa haki zao kwa upande wa kisiasa na kuweza kushiriki kugombea nafasi za uongozi katika kugombea .
 
Alisema katika harakati za kulilia ukombozi wa mwanamke umezidi kufanya kazi hususani katika suala la ufuatiliaji wa haki za binaadamu ik,iwa ni pamoja ya kuchagua na kuweza kuchagulia kwa mujibu wa sheria.
 
Semina hiyo ya  siku tatu iliyofadhiliwa na  shirika la umoja wa Mataifa linalosaidia maendeleo ya wanawake (UNWOMEN) liliwashirikisha Waratibu wa vikundi  30 kutoka katika shehia mbali mbali za Mkoa wa Kaskazini Pemba .

 Na Zuwena Shaaban-Pemba    

0 comments:

Post a Comment

 
Design by M.S Chopoti | Bloggerized by Ulimwengu Wa Digital