Thursday, December 13, 2012

Wanafunzi Kiu waandamana, wagoma

Wanafunzi Kiu waandanana, wagoma


Mkuu wa Mkoa wa dare s Salaam, Said Meck Sadiki
 
Wanafunzi  wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala (Kiu) wameanzisha wamandamana na kugoma wakitaka ada ipunguzwe na watimiziwe mahitaji mbalimbali.

Mgomo huo umesababishwa na wanafunzi kutozwa ada kubwa bila kujulikana pesa hizo zinapoenda. Wahadhiri wao waligoma kufundisha kwa wiki nne zilizopita walishinikiza kulipwa mishahara yao hatua iliyosabanisha kuhairishwa kwa mitihani.

Juzi wanafunzi waliandamana na baadaye kugoma baada ya uongozi wa chuo kushindwa kuwapa ushirikiano. Waliandamana kuandamana na kufunga barabara ya Pugu ili kilio chao kisikike.

Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa dare s Salaam, Said Meck Sadiki, alilazimika kufika chuoni hapo juzi ili kusikiliza malalamiko ya wanafunzi hao.

Sadick alipofika chuoni hapo, wanachuo walimzuia kuingia kwenye ofisi za utawala wa chuo kwa madai kuwa angeelezwa uongo kama walivyodanganywa maofisa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ili asiweze kusikiliza kero zao.

Wanafunzi hao walimpeleka Sadiki katika eneo waliloliandaa na kumweleza malalamiko yao huku wakisisitiza kuwa uongozi wa chuo umepiiza kwa muda mrefu kutatua kero zao.

“Tulishawahi kwenda kuongea mpaka na TCU na Wizara ya Elimu ila walipokuja kuzungumza na uongozi wa chuo iliishia chini chini, hatukupewa majibu yoyote. Walibadili ada kutoka kwenye mfumo wa fedha za Dola kwenda kwenye fedha za kitanzania bila kupunguza hata Shilingi moja,” alisema Neema Mwandri, anayechukua Shahada ya Usimamizi wa Masoko.

“Sisi tunashangaa badala ya kupunguziwa ada tunaona ndo kwanza wanaleta walimu wapya 30 kutoka Uganda, sasa tunachojiuliza ni kwamba hawana hela za kutimiza haja zetu na kupunguza ada au wamegoma tu kutusikiliza,” alisema.

“Nimesikia kilio chenu na suala la uongozi wa chuo chenu kubadili fedha kutoka kwenye mfumo wa Dola kuwa za kitanzania badala ya kupunguza ada walitaka kuwafanyia kiini macho wakijua hamtaelewa, kumbe kuna wasomi hapa. Mimi kama Mkuu wa Mkoa, naahidi kufanyia kazi malalamiko yenu,” Sadiki aliwaambia wanachuo hao na kuongeza:

“Nipeni kati ya siku mbili hizi ili nifikishe malalamiko yenu kwa Waziri Mkuu na serikalini kwa ujumla,” aliongeza.


CHANZO: NIPASHE

0 comments:

Post a Comment

 
Design by M.S Chopoti | Bloggerized by Ulimwengu Wa Digital