Saturday, December 15, 2012

WATAALAMU WA FANI ZA UANDISHI TUMIENI VYEMA KALAMU ZENU

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI MH.MOHAMED SAID AMEWATAKAWANATALUUMA WA FANI YA UANDISHI WA HABARI KUZITUMIA VIZURI KALAMU ZAO KATIKA TASNIA HIYO KWA LENGO LA KUEPUSHA MIGOGORO INAYOWEZA KUJITOKEZA KATIKA JAMII INAYOSABABISHWA NA UANDISHI USIOZINGATIA MIKO NA MAADILI YA TAALUMA HIYO. HAYO AMEYASEMA WAKATI AKIZUNGUMZA KATIKA MAHAFALI YA NNE YA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA MAWA SILIANO YA UMMA ZANZIBAR YALIYOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA UKUMBI WA BARAZA LA WAWAKILISHI LA ZAMANI MNAZI MMOJA. AMESEMA TASNIA HIYO IKITUMIWA VIZURI KWA KUELIMISHA,KUHABARISHA NA KUBURUDISHA ITASAIDIA KUCHOCHEA MAENDELEO YA TAIFA KWANI WANATAALUMA WAKITOA TAARIFA SAHIHI ZILIZOFANYIWA UTAFTI WA KINA ZINAWEZA KUSAIDIA MIPANGO YA MAENDELEO YA TAIFA. AIDHA MH.MOHAMED AMEFAHAMISHA KUWA SERIKALI ITAJITAHIDI KUONA CHUO HICHO KINAKUWA PAMOJA NA KUYATAFUTIA UFUMBUZI MATATIZO YANAYOKIKABILI CHUO HICHO YAKIWEMO UHABA WA MADARASA,VIFAA VYA KUJIFUNZIA PAMOJA NA UKOSEFU WA MAJENGO YA KUDUMU YA CHUO HICHO. NAE KAIMU MKUU WA CHUO HICHO BW.RASHID OMAR KOMBO AMESEMA MIONGONI MWA MAFANIKIO YALIYOFIKIWA NA CHUO HICHO NI KUONGEZEKA KWA IDADI YA WANAFUNZI AMBAPO JUMLA YA WANAFUNZI WAPATAO 136 WA NGAZI YA STASHAHADA NA CHETI WA FANI UANDISHI WA MAGAZETI ,MAWASILIANO YA UMMA NAUTANGAZAJI WA REDIO NA TV WAMETUNUKIWA VYETI VYAO . KATIKA RISALA YA WAHITIMU WA CHUO HICHO WAMEISHUKURU SERIKALI YA JAMHURI YA WATU WA CHINA KWA KUTOA MSAADA WA KITAALUMA IKIWA NI PAMOJA NA KUWAFUNDISHA WANAFUNZI HAO LUGHA YA KICHINA. WANAFUNZI HAO KATIKA RISALA YAO WAMEYATAJA MATATIZO YANAYOWAKABILI IKIWA NI PAMOJA NA UKOSEFU WA MIKOPO KUTOKA SERIKALINI ILI IWASAIDIE KULIPIA ADA ZA CHUO KAMA ILIVYO KWA FANI NYINGINE ZINAZOPEWA MIKOPO. WAMESEMA KUWA MATATIZO MENGINE YANAYO WAKABILI NI PAMOJA NA UKOSEFU WA MAJENGO YA KUDUMU, UHABA WA MADARASA NA VIFAA VYA KIJIFUNZIA PAMOJA NA UHABA WA WAALIMU JAMBO AMBALO LINAKWAMISHA MAENDELEO YA KITAALUMA YA CHUO HICHO.

0 comments:

Post a Comment

 
Design by M.S Chopoti | Bloggerized by Ulimwengu Wa Digital