Kauli hiyo ameitoa leo katika uzinduzi wa bodi mpya chuo cha uandishi wa habari na mawasiliano ya umma Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa chuo hicho Vuga Mjini Unguja.
Mh-Mbarouk ameseman hayo leo tarehe12/12/1202 wakati alipokuwa akiizindua rasmi bodi mpya ya chuo hicho yenyen lengo la kukuza na kuimarisha mazingira bora ya chuoni hapo ili chuo hicho kiweze kuzalisha wasomi bora katika tasnia ya habari na wenye kuchochea upeo wa maendeleo hasa katika upande wa Uchumi wa chi yetu.
Pia amesema,changamoto kubwa zinakikumba chuo hicho ni kutokua na madarasa ya kutosha pamoja na ofisi ya kutendea kazi,hivyo ameitaka bodi hiyo mpya kutilia mkazo masuala hayo ili kupatikane mazingira mazuri yenye kuleta matarajio mema katika maendeleo ya chuo hicho.
Nae kwa upande wake mwenyekiti mpya wa bodi hiyo Nd-Chande Omar Omar asema,kupitia wajumbe wenzake watachukua jitihada mbadala za kuweza kuweka mazingira safi Pamoja na upatikanaji wa elimu iliobora chuoni hapo kwa kuzingatia sheria na kanuni za chuo hicho.
Aidha ameendelea kusema kuwa kwa kushirikiana na wizara ya habari bodi hio watatafuta wafadhili mbalimbali watakao weza kuleta maendeleo ya chuo hicho.
Sambamba na hayo ametoa shukradhi za dhati kwa waziri huyo kwakuweza kuungana pamoja kutekeleza kazi zao ambazo zinalenga kuweka mazingira bora ya chuo hicho.
Bodi iliopita imekwisha muda wake tarehe 9 june mwaka huu,na bodi mpya imezinduliwa leo tarehe 12/12/1012 ambayo inawajumbe kadhaa miongoni mwa wajumbe hao ni mkurugenzi wa Idara ya habari maelezo Zanzibar Nd,Yussuf Omar Chunda,Bi Najma khalfan na wengineo, pia hafla hio ilihudhuriwa na walimu na baadi ya wanafunzi wa chuo hicho.
0 comments:
Post a Comment