Akitangaza rasmi maamuzi yalioamuliwa na kikao cha Kamati Utendaji ya ZFA kilichofanyika ofisi za chama hicho zilizopo Kiembe Samaki wilaya ya mjini magharib,Makamu wa Rais wa ZFA Alhaj Haji Ameir, alisema kuwa Wajumbe wote wa Kamati ya tendaji walioshiriki kikao hicho kwa pamoja wameunga mkono suala hilo, kwani wamesema litakuwa fundisho kwa wachezaji wengine wanaokuja.
Kikao hicho cha dharura kimefanyika kufuatia sakata la wachezaji wa Zanzibar Heroes kuamua kugawana kiasi cha dola za Kimarekani 10,000 walizopata baada ya kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge iliyomalizika wiki iliyopita mjini Kampala, Uganda, baada ya kuifunga Bara, Kilimanjaro Stars kwa penalti 6-5, kufuatia sare ya 1-1.
Inaaminika kuwa wachezaji hao waliamua kugawana fedha hizo kwa madai kuwa chama cha soka znz kimekuwa hakiwatendei haki na ni mara nyingi wamekuwa wakiwadhulumu pesa zao.
0 comments:
Post a Comment